Kilimanjaro Rangers ilianzishwa mwaka 2010 chini ya uongozi wa mwenyekiti Adam Aweso Kipacha na marafiki zake ikifadhiliwa na Bw. Mussa Ally.
Timu ilianzishwa ili kuleta mabadiliko ya mpira wa miguu katika mkoa wa Kilimanjaro kwani kwa kipindi hicho kulikuwa hakuna timu inayocheza ligi kuu kutoka Mkoa wa Kilimanjaro. Tatizo kubwa ilikuwa ni fedha na hakuna mchezaji yeyote aliyekuwa analipwa kwani hata usafiriwa timu ilikuwa tabu. Wachezaji walihamasihwa kuchangia timu ili kuisaidia.
Timu ilishiriki katika ligi ya wilaya mwaka huohuo iliyoanza 25/09/2010 na kumalizika 25/10/2010. Timu ilianza vyema kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Railway na kutoka sare 2-2 na timu ya Bonite.Iliendeleza ushindi wake kwa timu ya Mnazi na kufuzu kuingia hatua ya robo fainali.
Mafanikio
1. KRFC ilifanikiwa kuwa timu bora, timu yenye nidhamu na kutoa mchezaji bora wa mashindano katika mashindano ya MKOMBOZI CUP mwaka 2011.
2. Toka timu ya USHIRIKA kutolewa ligi kuu KRFC ndio timu pekee iliyoweza kuleta timu yenye jina kubwa SIMBA SPORTS CLUB wenye umri chini ya miaka 23 kucheza nayo katika uwanja wa Ushirika Moshi japo ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa 4 - 1
3. KRFC iliweza kuandaa michuano ya soka umri chini ya miaka 20 (16.09.11 hadi 23.09.11) na kushirikisha timu za Arusha FC ya Arusha, Simba FC ya Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, AMANI ya Moshi, Machava ya Moshi na wenyeji KRFC. Katika mashindano hayo KRFC ilipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Arusha FC kwa 4 - 1 na kufanikiwa kushinda mchezo wake wa pili dhidi ya Machava kwa 1 - 0.( Kwa sasa michuano hiyo bado inaendelea)