Featured Posts

Monday, September 10, 2012

JEZI ZA MAZOEZI

Hizi ndio jezi zetu za mazoezi mwaka huu 2012.

Saturday, August 11, 2012

KRFC kucheza fainali MKOMBOZI CUP leo

Timu ya Kilimanjaro Rangers FC leo itaingia uwanjani kucheza na Kitayosa
FC katika fainali ya MKOMBOZI CUP. Timu hiyo inayopewa nafasi ya kuchukua
kombe hilo ilizitoa timu za Machava katika robo fainali na kuitoa timu ya
TPC kwenye nusu fainali za mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja
vya Memorial mjini Moshi.

Friday, August 10, 2012

African Lyon yapata kocha mpya kutoka Argentina

Timu ya African Lyon imepata kocha mpya kutoka Argentina,Pablo Ignacio Velez na ameshawasili nchini tayari kuanza kuinoa timu hiyo na kuomba apewe muda wa kukisuka upya kikosi hicho huku akiahidi mabadiliko zaidi ya soka kwenye timu hiyo.

Friday, July 13, 2012

SIMBA YATWAA KOMBE LA URAFIKI UWANJA WA TAIFA

Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati,  baada ya kutoka suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri na wa kuvutia kwa timu zote uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo hivyo kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.


Wachezaji wa timu ya Simba pamoja na kocha wao wakipiga picha pamoja na kombe lao walilolikabidhiwa leo kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika michuano ya Urafiki inayoandaliwa visiwani Zanzibar.

Wachezaji wa timu ya Simba wakisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuchukua ubingwa wa kombe la Urafiki.

Wachezaji wa timu ya Azam FC nao wakisalimiana na viongozi mpira wa miguu kutoka Zanzibar pamoja na mgeni rasmi.

Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa.

Wachezaji wa timu ya Simba wakimnyanyua juu juu golikipa wao Juma K. Juma baada ya kupangua penati mbili katika mchezo huo uliokuwa wa fainali katika michuano ya Urafiki.

Ubao wa matangazo ukionyesha Simba 5 Azam FC 3 kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezaji wa kimataifa wa timu ya Simba kutoka nchini Zambia Felix Sunzu akichuana vikali na beki wa timu ya Azam FC katika mchezo huo.

Mashabiki wa timu ya Azam FC wakishangilia timu yao.

Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.