Tuesday, July 12, 2011

Maradona apata ajali

Mchezaji mashuhuri na aliyekuwa kocha wa Argentina Diego Maradona na mwenza wake Veronika Ojenda wamepelekwa hospitali baada ya gari walilokuwa wakitumia kupata ajali lilipogongana na basi mjini Costa Rica. Maradoma amesema kuwa ameumia goti na mwenza wake paja. Meneja wa Hospitali alipolazwa bwana Oscar Sico amesema kuwa majeruhi hao wapo katika hali nzuri na wanaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani. Chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa

No comments:

Post a Comment