Saturday, September 17, 2011

AMANI CENTRE YAWAFUNDISHA SOKA COASTAL UNION

Timu ya Soka ya vijana  AMANI CENTRE ya mjini Moshi leo imewafundisha soka timu ya vijana wenzao wa COASTAL UNION ya mjini Tanga baada ya kuwanyuka 2 – 1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ushirika Moshi. Huu ni mchezo wa pili katika mashindano ya vijana yaliyoandaliwa na timu ya KILIMANJARO RANGERS baada ya ule wa jana kati ya ARUSHA FC na KILIMANJARO RANGERS uliomalizika kwa wenyeji kupigwa 4 – 1. Kesho michuanao hiyo itaendelea  kwa michezo miwili kati ya KILIMANJARO RANGERS dhidi ya MACHAVA utakaopigwa saa nane za mchana utakaofuatiwa na SIMBA SC dhidi ya COASTAL UNION.

No comments:

Post a Comment