Friday, July 15, 2011

Arsenal Yaua

Arsenal imeanza ziara yake barani Asia kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya nyota wa Malaysia iliyofanyika kwenye Uwanja wa  Taifa wa  Bukit Jalil.

Gunners ilicheza mechi yake ya kwanza nchini Malaysia baada ya kupita miaka12, ilitawala mchezo huo kuanzia mwanzo hadi mwisho, huku kocha Arsene Wenger akiwatumia wachezaji chipukizi mwanzo na kipindi cha pili akiwaingia nyota wake.

Beki wa kushoto Kieran Gibbs alionyesha kiwango kizuri cha kumvutia Wenger kufutia kuondoka kwa Gael Glichy, lakini uchezaji wa beki wa kulia wa akiba Carl Jenkinson ulimfanya kocha huyo Mfaransa kutingisha kichwa.

Beki huyo chipukizi alikuwa na kazi kubwa ya kumzuia winga mwenye kasi kubwa wa Malaysia, S. Kunalan, aliyejaribu kutengeneza nafasi nyingi, japokuwa beki ya Gunners ilikuwa makini.

Viungo chipukizi wa Arsenal, Jack Wilshere na Aaron Ramsey walitawala sehemu ya kiungo.

No comments:

Post a Comment