Timu ya soka ya Kilimanjaro Rangers ya Mjipya Moshi, kesho itajitupa uwanjani kujipima nguvu na timu ya SIMBA B katika uwanja wa Ushirika mjini moshi. Akithibitisha kwa tovuti hii mwenyekiti wa Kilimanjaro Rangers bw. Adam Kipacha amesema kuwa mechi itakuwepo na itachezwa kuanzia saa kumi kamili za jioni. Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 500 za Kitanzania hivyo amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuangalia maendeleo ya soka ya timu yao. “Tumejipanga vizuri, licha ya kutolewa na TPC katika mashindano ya Mkombozi cup ila tulionyesha soka safi na hata kuwa timu bora ya mashindano” alisema mwenyekiti huyo. Amesema licha ya mechi hiyo kuja ghafla lakini watu wa Moshi wategemee burudani kali kutoka kwa KRFC.
Tuesday, July 19, 2011
KILI RANGERS KUCHEZA NA SIMBA B KESHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment