Sunday, July 24, 2011

KILI RANGERS KUKIPIGA NA FOREST WIKI IJAYO

Timu ya Kilimanjaro Rangers FC itajitupa uwanjani na timu ya FOREST ya mjimwema jumamosi ya wiki ijayo katika kombe lililoanzishwa na mlezi wa timu hiyo lijulikanalo kama KILICUP. Akiongea na mtandao huu mlezi huyo alisema kuwa "Nataka tucheze mechi nyingi kadiri tuwezavyo, malengo yetu ni kukuza soka la Kilimanjaro hivyo kutegemea mashindano ya msimu hatuwezi kukuza soka. Kwa sasa tunatambulisha uwepo wa Kombe hili na tutafanya hivi kwa mfululizo wa miezi mitatu kabla hatujaamua kucheza mfumo wa ligi. Kuendesha ligi ni gharama hivyo basi ni jukumu letu kutambulisha kombe hili, kuwavuta wadau na tujadiliane timu zitakazoshiriki mfumo wa ligi. Mfumo wa ligi huzipa timu nafasi ya kurekebisha makosa na pia huzipa timu mechi nyingi sana za kucheza hivyo kuzoea mechi na kujiweka vizuri. Timu zetu kama hamna mashindano huwa zinazembea mazoezi hivyo kwa kuanzisha kombe hili nadhani mpira utakuwa." Kombe hilo licha ya kuanza na zawadi ndogo zinatazamiwa kukua kadiri siku zinavyokwenda.

No comments:

Post a Comment