Wednesday, July 20, 2011

KILI RANGERS YAPOKEA KICHAPO 4 - 1

Timu ya Kilimanjaro Rangers imepokea kichapo cha 4 – 1 kutoka kwa kikosi cha timu ya SIMBA B. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa KRFC amesema kuwa timu yake imejitahidi, na imejisikia fahari kucheza na timu yenye jina kubwa. “Ingawa hatujafurahishwa sana na matokeo ila tumejitahidi, tumejifuunza mengi. Wachezaji wetu wamekosa exposure na hili ndio tunalifanyia kazi kwani sisi bado ni wachanga sana katika soka.” Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa SIMBA wamesema kuwa walijua watashinda, “Tulijua tutashinda, tena kwa ushindi wa zaidi ya goli kumi ila vijana wamejitahidi kiasi chao na wamefika langoni kwetu mara nyingi, tunapenda kuwaomba wakae pamoja na wafanye mazoezi ya physical labda hayo ndo mapungufu.

Mbali na mchezaji mmoja wa Kilimanjaro Rangers kupewa kadi nyekundu wenyewe wamesema kuwa wamefarijika na wamefurahi kuandaa na kufanikisha kucheza mchezo huo.

 

No comments:

Post a Comment