Wednesday, July 20, 2011

NGASA KUKIPIGA NA MAN U

Hii leo tarehe 20 kwa masaa ya Marekani ambako itakuwa siku ishabadilika kwa masaa ya Afrika Mashariki na kuwa tarehe 21, Ngassa anatarajiwa kucheza katika mpambano dhidi ya Manchester United baada ya kufanya vyema katika majaribio yake katika klabu ya Seattle Sounders.

Kwa mujibu wa taarifa ilizozinasa mtandao huu kutoka katika mitandao mbalimbali ya Marekani Ngassa atakuwa mchezaji pekee aliyopo katika majaribio atakae pata nafasi ya kucheza dhidi ya Mashetani wekundu wa Old traford ikiwa ni mahali pakumuangalia vyema kabla ya kuingia katika biashara ya kumchukua.

Ngassa kama atapata nafasi kama mitandao inavyo eleza atakuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza dhidi ya mabingwa hao wa Uingeleza.

No comments:

Post a Comment