Monday, September 5, 2011

TWIGA STARS YAPOTEZA, YAPIGWA 1 - 2 NA GHANA

Timu ya wanawake ya Taifa ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza mechi yake
ya kwanza ya michezo ya All Africa Games (AAG) baada ya leo kufungwa mabao
2-1 na Ghana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machava, jijini Maputo.
Kwa mujibu wa Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis hadi mapumziko timu
hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Mwanahamisi Shuruwa aliisawazishia Twiga
Stars dakika ya 85, lakini Ghana ikapata bao la pili dakika tatu kabla ya
filimbi ya mwisho.
Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili Septemba 8 mwaka huu dhidi Afrika
Kusini. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi itakuwa Septemba 11
mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment