Friday, November 4, 2011

Samata aweka recodi afunga 6 dhidi ya FC Police

TP Mazembe imetoa kichapo kitakatifu kwa timu ya FC Police cha magoli 13-1 katika michuano ya ligi kwa jimbo la Katanga.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya TP Mazembe leo amefanya maajabu makubwa katika historia ya soka la nchini Congo baada ya kufunga magoli 6 kati ya 13 yaliyowekwa kimiani na TP dhidi ya FC Police katika michuano ya ligi ya jimbo la Katanga. Katika Mchezo huo ulishuhudia Mtanzania Mbwana Samata akiweka rikodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kufunga magoli 6 katika mchezo mmoja, huku magoli mengine yakifungwa na Lusadisu aliyefunga matatu, Kanteng aliyefunga mawili na Mabele.Samatta anamiezi 6 tangu ajiunge na TP Mazembe akitokea Simba ambako alicheza mzunguko mmoja (miezi 4) na kueleke Congo kwa TP Mazembe.

No comments:

Post a Comment