Sunday, July 31, 2011

MAN U YAICHAPA BARCA

Timu ya Manchester United imeifunga timu ya Barcelona 2 – 1 katika mechi yao ya kirafiki. Man U ndio walikuwa wakwanza kuandika goli kupitia kwa mchezaji wake machachari kutoka Ureno NANI dakika ya 22 tu ya mchezo. Mchezo ulienda mapumziko Man U wakiongoza 1 – 0. Kipindi cha pili kilianza kwa soka safi lililoonyeshwa na timu zote mbili, na manamo dakika ya 70 Alcantara aliisawazishia BARCA. Ni dakika 6 tu baadae Oweni akaiandikia MAN U bao la pili na la ushindi hivyo kuvunja uteja wa timu hiyo kufungwa na BARCA

No comments:

Post a Comment