kumpunguzia mashaka mlinda mlango wa Manchester United David de Gea,
wakati Manchester United walipoanza kampeni ya kuutetea ubingwa wake kwa
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Brom.
Wayne Rooney alifunga bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza baada ya
kugongeana vizuri na Fabio pamoja na Ashley Young na kuachia mkwaju
uliomshinda mlinda mlango wa West Brom Ben Foster.
Shane Long akasawazisha katika mechi yake ya kwanza kubwa kwa klabu ya
West Brom baada ya mkwaju wake hafifu kupita kwapani mwa mlinda mlango De
Gea.
United walipata bao la ushindi baada ya krosi iliyopigwa upande wa kushoto
na Ashley Young ikamgonga mlinzi wa West Brom Steven Reid mpira ukajaa
wavuni na kumuacha mlinda mlango Ben Foster asijue la kufanya.
Matokeo hayo yameifanya Manchester United kushika nafasi ya pili ikiwa na
pointi tatu nyuma ya vinara wa ligi hadi sasa Bolton wenye pointi tatu na
mabao manne ya kufunga.
No comments:
Post a Comment